NAIBU WAZIRI ULEGA AJIBU MASWALI MAGUMU YA WAVUVI TOKA VISIWANI.

Naibu waziri wa mifugo na uvuvi nchini Tanzania mheshimiwa Abdallah Ulega amewataka wavuvi wa dagaa,  kutoka Tanzania visiwani kufuata sheria za uvuvi zilizopo tanzania bara na kwamba hakutakuwa na mtu atayewazuia kuvua.

Mheshimiwa Ulega ametoa kauli hiyo kufuatia baadhi ya wavuvi kulalamikia hoja ya kukata leseni wanapofika Tanzania Bara pamoja na kupigwa marufuku kutumia nyavu zenye matundu ya MM6 ambazo huruhusiwa kutumika Zanzibar.

Utuondole hofu sisi wananchi wako hizi nyavu zetu kule kwetu huwa ni milimita 6 na 8 tunazitumia na serikali imeruhusu”

Vifaa vyote vya uvuvi maboti na nyavu zinatoka vinatokea kwa wenzetu hapo pemba na  Zanzibar lakini mtu yule akitoka akiingia ardhi ya pangani basi utasikia lete leseni unapeleka lakani waambiwa hii leseni haitakiwi sasa Tanzania na Zanzibar ni tofauti kuna maana gani hii kuitwa Tanzania siingeitwa Tanganyika tu

Akijibia malalamiko hayo mh.ulega amewasisitiza wavuvi hao kufuata sheria zilizopo huku serikali ikiendelea kufanya uchunguzi kwa kuwa  suala la uvuvi halipo katika muungano.

fuateni utaratibu na mmeruhusiwa kufanya kazi sehemu yoyote hapa nchini hii sisi huku tunaendeeshwa na sheria inayosema vyavu sahihi ni za milimita 8 kwenda juu lakini sasa hio mililita 8 ilinganishwe na hio ya zanzibari hatufanyi sisi maamuzi ya hapo kwa hapo ni lazima tukae tufanye utafiti wa kisayansi tukubaliane na tuipitishe au tuikatae kwakuwa ile sheria ya kule na yahuku zinagongana yule mtanzania akija huku ni lazima apokelewe na afate utaratibu wa huku haruhusiwi kuvua lakini afate utaratibu na viongozi niwaombee mvuvi akifuata utaratibu msimpige mikwara ikiwa wamefuata utaratibu wa kisheria wapokeeni

Miongoni mwa viongozi waliokuwepo katika mkutano huo ni Mbunge wa jimbo la Pangani ambaye ni NW M mheshimiwa jumaa Hamidu aweso ambapo amemuomba Mheshimiwa Ulega kuangalia uwezekanao wa kujenga bandari ya uvuvi pamoja msaada wa vifaa vya uvuvi.

Mh naibu waziri ukiangali huu wote ni ukanda wa bahari tuangalie namna ya kujenga bandari ya uvuvi ili wavuvi hawa waweze kunufaika tunaweza tukawa na bahari lakini bila ya nyenzo tunaweza tusitoke mh naibu waziri leo tunaomba utuambie zahiri shairi ni namna gani wavuvi wa pangani wanaweza kufaidika na nyenzo hizi” ……….alisema mbunge wa jimbo la pangani MH Jumaa Aweso

Kutokana na ombi hilo Mheshimiwa Ulega ameahidi kuleta mashine za boti zitakazotolewa kwa baadhi ya vikundi vya wavuvi vuilivyo hai huku akiwaagiza mkuu wa wilaya kuhakikisha ushirika wa wavuvi wilayani Pangani unakuwa hai.

na mimi nataka niwaambie kwamba  mbunge namkuu wa wilaya ushirika ufufuke  na mimi nitahakikisha ninawaunga mkono wa kuwaletea mashine za boti kwa ajili ya wanachama wa ushirika waliohia ila kwa leo siwaambii ni mashine ngapi ntawaletea ili hii pangani isonge mbele”……alisema naibu waziri wa mifugo na uvuvi

Hayo yamejiri leo katika ziara ya siku moja ya naibu waziri wa Mifugo na uvuvi Mheshimiwa Abdallah Ulega wilayani Pangani ambapo katika ahadi zake amesema baada ya soko hilo kukamilika ujenzi wake wataleta jokofu pamoja na kuichukua changamoto ya tozo kubwa ya dagaa na kuijadili bungeni .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *