WAUZA SUKARI BEI YA JUU PANGANI KURIPOTIWA POLISI NA WATEJA WAO.

Wafanyabiashara wilayani Pangani mkoani tanga wametakiwa kufuata agizo la serikali la kuuza sukari kwa bei elekezi ya shilingi 2700 badala ya kuutumia mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani kuwapandishia wananchi bei kwani kufanya hivyo ni kukiuka sheria na atakaebanika atachukuliwa hatua .

Wito huo umetolewa na afisa biashara wilaya Pangani bwana Mohamed Hussein ambapo mbali na kuwataka wafanyabishara kuuza sukari kwa bei elekezi ,amewasisitiza wananchi kutoa taarifa jeshi la polisi endapo kutakuwa na mfanyabiashara  anaekiuka agizo hilo.

“Wafanyabiashara  wafuate sheria bila shuruti kwa sababu serikali ilishafanya research na kujua bei ya sukari.. wasitumie mfungo huu wa ramadhani kuwabambikia bei wananchi  atakekiuka na maagizo  atakumbana na sharia na wananchi wasisite kutoa taarifa jeshi la polisi au halmashuri endapo watauziwa sukari kinyume na bei elekezi’Amesema Bwana Mohamed (Afisa Biashara Wilaya)

Aidha bwana Mohamed amesema kuwa kwa wilaya ya Pangani bado kunachangamoto ya utekelezaji wa agizo hilo kutokana na  wafanyabiashara kudai kuwa  wamenunua sukari kwa bei ambayo inawalazimu kuuza shilingi 3200  na kusisitiza kuwa atakaekiuka agizo la serikali atapigwa faini

“kwa hapa Pangani bado kuna ugumu kwa baadhi ya wafanya biashara bado wengine  wanauza shilingi 3000 na 3200  wengi wanadai waliponunua kwa wafanyabiashara wa jumla wanalazimika kuuza bei hiyo ..na tuna mikakati ya kupita kijiji kwa kijiji  tuweze kuwapa elimu juu ya bei elekezi  na tangazo la serikali limesema wazi atakekiuka tapigwa faini “

Katika hatua nyingine bwana Mohamed amesema tayari serikali imeleta sukari  takribani tani   22,000 ambazo wafanyabiashara watanunua na kuuza kwa bei elekezi ya shilingi 2700 kwa mkoa wa tanga

Mnamo tarehe 24.4.2020  serikali ilitangangza bei elekezi ya sukari kupitia gazeti la serikali no 284 ambapo bei elekezi ya sukari kwa mkoa tanga ni shilingi 2700

GAZETI LA SERIKALI   NO 284  TARE 24.4.2020 BEI ELEKEZI 2700