MZAZI MPE MTOTO RADIO DARASA LIENDELEE

Wazazi na walezi wilayani Pangani mkoani TANGA wametakiwa kuwasimamia watoto wao ambao ni wanafunzi ili waweze kuitumia fursa ya uwepo wa kipindi cha RADIO DARASA kinachorushwa na kituo hiki ili  kujifunza masomo mbali mbali katika kipindi hiki ambacho wamelazimika kubaki nyumbani kutokana na Janga la Corona.

Hayo yamejiri leo katika uzinduzi wa kipindi hicho uliofanyika katika kipindi cha Asubuhi ya Leo kinachorushwa na Pangani FM.

Akizungumza katika kipindi hicho kaimu afisa elimu shule za Sekondari bwana ALLY MWICHAGA Ametoaa wito kwa wazazi kuwarudisha nyumbani watoto waliokwenda kujishuhulisha na shughuli mbali mbali ili washiriki vipindi vitakavyorushwa kupitia kipindi maalumu chenye Lengo la kuwawezesha wanafunzi kujifunza kupitia Radio.

’wito wangu kwa mzazi hakuna kitu kikubwa kama kumuelekeza kijana wanafunzi hawa haswa wa sekondari ni wanafunzi wakubwa inawezekana kuwa wamekwenda kwenye uvuvi huko au mashambani sasa katika kipindi hiki cha radio darasa ningependa kutoa wito kwa wazazi kwamba watoto wote warudi nyumbani kwa sasabu vipidi vinaanza leo wanafunzi wasikose warudi nyumbani na wazingatie ni nini kinafundishwa’’ – Bw. Mwichaga

Bi Mariheta Hipolite ni Afisa Elimu taaluma shule za msingi wilayani hapa ,amewataka wazazi kutoa ushirikiano kwa watoto wao kwa kuwapatia vifaa vitakavyowezesha kujifunza na kuhakikisha wanazingatia masomo hayo sambamba na kusimamia nafasi yao kwa kuwalinda ili kuwaepusha na maambukizi ya virusi vya corona.

’wito wangu mimi ni kwa wazazi ninachoomba tutoe ushirikiano hasa watoto wangu hawa wa shule za msingi ni wadogo sana kwa hiyo wazazi wahakikishe mtoto anazingatia suala la elimu, tutakuwa hatujatenda haki sana kama wadau waliotupa hiki kipindi tena bila malipo kurusha matangazo ya kufundisha Halafu sisi wazazi tukawalemaza watoto kwa kutozingatia kile kinachofundishwa, tuwape ushirikiano kwa kuwapa vifaa kama Simu kwa ajili yakuuliza maswali na Radio kwa ajili ya kusikiliza, na tusiruhusu mtoto akakuaga kuwa anakwenda kusikiliza radio kwa jirani ni jukumu letu kuwalinda pia na maambukizi ya corona kwa kuepusha mikusanyika isiyo ya lazima, mtoto wa kike ni jukumu letu kumlinda ili asikumbane na mabaalaa huko atakakokwenda’’ amesema marieta.

Kwa upande wa Meneja wa Pangani fm Radio Bi. maimuna msangi amesisitiza jukumu la mzazi au mlezi kuwatengea muda wa kujisomea watoto wao kwa kuwapa ushirikiano na kumkumbushia kufanya kazi za shule walizopatiwa.

‘’jambo lolote ili liweze kufanikiwa linaitaji mihimili kwa watu wa pande zote kuhakikisha jambo linakuwa kamili mwalimu anapotoa kazi ya shule anamtegemea mzazi atachukuwa nafasi yakumuhimiza ili aifanye kazi yake kwa ufasaha, mwalimu atafanya jukumu lake na mzazi uchukuwe jukumu lako ili mtoto aweze kufanikiwa’’ amesema maimuna.

Nao baadhi ya walimu waliopata nafasi ya kufundisha wanafunzi kupitia kipindi cha Radio Darasa wameelezea namna walivyoguswa na kipindi hicho huku wakieleza utofauti uliopo kati ya ufundishaji wa radioni na darasani na kuelezea manufaa watakayoyapata wanafunzi endapo watazingatia masomo hayo.

’baada ya kusikia hili suala la kufundisha mimi nilishtuka sana unajuwa kuna utofauti kati ya ufundishaji wa darasani na ufundishaji wa radioni ukiwa mnatazamana na mwanafunzi akicheza unamjuwa lakini kupitia radio ni ngumu kujuwa nani yupo pamoja na wewe, niwaombe wanafunzi wazingatie masomo yanayotolewa na walimu kupitia kipindi hiki’’ mmoja wa walimu.

Kipindi cha Radio Darasa kina ni Kipindi Mahsusi chenye lengo la kuwawezesha wanafunzi ambao wamelazimika kuwepo nyumbani kutokana na Janga la Corona kuweza kujifunza kupitia Radio.