Mkuu wa mkoa Tanga Martin Shigela ameipongeza halmshauri ya Wilaya Pangani kwa kusimamia ukusanyaji wa mapato hali iliyopelekea kupata hati safi
Kukulingana na ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha wafedha 2018 /2019
Shigela ameyasema hayo wakati wa kikao maalumu cha kujadili ripoti ya Mkaguzi na mdhibiti wa Hesabu za Serikali kilichofanyika katika ofisi ya za Halmasahuri ya Wilaya hiyo ambapo mbali na kuipongeza Halmashuri hiyo ameitaka kuweka utaratibu mzuri ya kulipa madeni wanayodaiwa sambamba na kumuagiza mkuu wa Wilaya kufuatilia takribani shilingi mil .61 wanazodaiwa watu ambao walipewa kazi ya kukusanya fedha
“kutokana na mapato haya hatutarajii madeni ya waheshimiwa madiwani kuendelea kuwepo wala mafao yao yachelewe kulipwa ..ningependa utaratibu mzuri uwekwe na ndugu zangu wanapangani tunajua tunadai na kudaiwa na kuna fedha zaidi ya mil.61 zipo kwa wakandarasi watendaji,na watumishi wa halamashauri ambao tuliwapa kazi ya kukusanya fedha ..mheshimiwa dc nakupa kazi hii hadi tarehe 15/06/2020 fedha hizo zirudishwe na wakishindwa tuwapeleke mahakamani kwa matumizi mabaya ya fedha za umma…dawa ya deni ni kulipa”
Aidha Bw. Shigela maewataka madiwani kuhakikisha wanasimamia suala la upatikanaji wa mikopo kwa vikundi vya Wanawake ,vijana na walemavu sambamba na kusimamia suala la urejeshaji wa Fedha walizokopa ili kila mmoja aweze kunufaika nazo
“mheshimiwa mwenyekiti kabla hamjamaliza wakati wenu jambo hili mlisimamie..kwanza mjue kati ya makusanyo ni kiasi gani cha fedha kilitakiwa kwenda kwenye mikopo ya wanawake ,vijana na walemavu..pili mfahamu kiasi gani cha fedha kimetoka ..tatu mfahamu vikundi vingapi vimeomba na vingapi havijapata …ili kila mmoja anufaike ..suala jingine nikurejesha fedha za mikopo tumekuwa hodari sana wakutoa mikopo lakini suala la ufuatiliaji wa kurejesha bado tuko nyuma..nielekeze vikundi vyote vilivyokopa wafanye utaratibu wa kurejesha ili kila mmoja anufaike’
Naye Mkuu wa Wilaya Pangani Bi Zainabu Abdallah amemuahidi Mkuu wa Mkoa kuendelea kuimarisha ukusanyaji wa mapato sambamba na kubuni vyanzo vipya vya mapato
“sisi pangani tulikua na changamoto kubwa sana mpaka januari makusanyo yalikua 28% baada ya kupata mashine hadi april makusanyo ni 68% kwa hiyo tunaona ni matokeo mazuri naomba ni kuahidi hadi kufikia Juni tuatafikia lengo la serikali na tutaimarisha vyanzo vya mapato na kubuni vyanzo vipya ili halmashauri yetu iweze kujiendesha “
Kwaupande wake katibu tawala mkoa wa tanga Bi ZIGITA OMARI mbali na kuwapongeza watumishi wa halmashauri kwa kazi nzuri amewataka kutobweteka na badala yake kuzifanyia kazi hoja ambazo hazijajibiwa kwenye Ripoti ya m
Mkaguzi na kuzingatia ukusanyaji wa mapato ya ndani ilikurahisisha uendeshaji wa halamshuri
Halamashauri ya Wilaya Pangani ilifanyiwa ukaguzi na CAG kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 na Ripoti ya ukaguzi ilikabidhiwa kwa Rais mwishoni mwa mwezi march 2020 ambapo Hamashauri ya Wilaya Pangani ilipata hati safi na katika taarifa ya Mkaguzi hoja 110 zilizobainishwa na hoja 63 bado hazijapatiwa majibu