SIKU YA HEDHI SALAMA 2020: TOZO KWENYE TAULO ZA KIKE BADO NI MWIBA KWA MABINTI.

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya hedhi salama duniani inayoadhimishwa kila tarehe 28 may, serikali imeombwa kutengeneza mazingira rafiki kwa wanafunzi wa kike wawapo mashuleni ili kuwawezesha hedhi salama huku wakiendelea na masomo yao

Hayo yamesema hii leo na Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Community Volunteer Services Tanzania [CVS-TANZANIA] bwana SAIMON MASHAURI ambapo ameiomba serikali kutengeneza mazingira yatakayowasaidia wanafunzi mashuleni kuwa huru na kuweza kujifunza wakiwa na Amani na furaha.

“serikali itengeneze mazingira rafiki kwa wanafunzi wakike kuwepo na vyumba vya kubadilishia nguo,maji safi na salama, vyoo bora, mtoto wa kike anatakiwa asikae sana pedi, masaa sahihi ya kukaa na pedi ni masaa sita au saba haizidi ikipita masaa hayo ni matatizo kwako hivyo srikali itoe fursa katika taasisimbalimbali.”

Aidha bwana MASHAURI ameitaka serikali kuondoa kodi za taulo za kike ili upatikanaji wake uwe rahisi na kuwafikia wasichana hususani wa vijijini na kuwataka wanaume kuwasaidia wanawake kununua taulo hizo kwaajili ya matumizi ya wanawake na wasichana

“niombe jamii hili suala ni la kila mmoja na serikali ilitazame jambo hili kwa jicho la tatu ikiwezekana itoe kodi ya taulo za kike ili zipatikane kwa urahisi, elimu inatakiwa itolewe sana kwa sababu hii sio starehe ni kitu amabcho ni muhimu sana kwa mtoto wa kike na msichana”

Bwana MASHAURI ameiomba serikali kuunga mkono na kutoa ruzuku kwa mashirika mbalimbali ambayo yanaanzisha kampeni za wasichana mashuleni ili kuongeza jitihada kwa taasisi na walengwa kwa ujumla.

“serikali tunaiomba kuangalia mashirika ambayo yanatoa elimu hii kuweza kutoa ruzuku na kuunga mkono yaweze kutoa elimu kwa walemavu na kuwapatia taulo wananfunzi ,wanawake au wasichana ili wawe na Amani hata anapotembea au awapoa darasani ajiamini kwamaba yupo huru na salama kiafya”

Kwa mujibu wa utafiti wa awali uliofanywa na NIMR unaonyesha ni asilimia 17 pekee ya shule nchini zina vyumba maalumu vya hedhi salama, huku asilimia 28 ya mabinti wanauwelewa juu ya hedhi salama na huku utafiti wa SNV uliofanyika katika wilaya 16 nchini unaonyesha zaidi ya asilimia 80 ya shule hazina miundombinu rafiki wa wanafunzi ikiwemo ukosefu wa maji safi na salama, matundu machache ya vyoo na ubovu wa milango.

Pia wengi hushindwa kumudu bei za kununulia vifaa vya kujistiri na kulazimika kukaa nyumbani kipindi cha hedhi. Na hivyo kukosa masomo