MTU MMOJA AMEKUFA MAJI BAADA YA KUTELEZA KWENYE NGAZI ZA CHOMBO CHA MAJI AKIWA AMELEWA

Jeshi la polisi Wilayani Pangani Mkoani Tanga limethibitisha kutokea kwa kifo cha kijana moja aliefahamika kwa jina la Erick Deogratus Jacob mwenye umri wa miaka 41 mfanyakazi wa chombo cha baharini.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mkuu wa upelelezi wilaya ya Pangani ASP MATIKU amesema kwamba tarehe 30 May mwaka huu majira ya saa tatu na nusu usiku marehemu alirudi katika chombo hicho akiwa amelewa na wakati anapanda ndipo alipoteleza na kuanguka katika maji.

Nathibitisha kwa kitokea kwa kifo cha kijana mwenye umri wa miaka 41 aliyefahamika kwa jina la Erick Degratus Jacob kabila lake msambaa ambae ni mfanyakazi wa chombo cha bahari jana majira ya saa tatu na nusu usiku alirudi kwenye chombo hiko akitokea kwenye maeneo ya starehe akiwa amelewa sana sasa wakati anapanda ngazi ya chombo hicho ndipo alipoteleza na kuangukia kwenye maji na kuzama majina mauti yakamfika hapo hapo .- ASP-MATIKU

Aidha ASP- Matiku ametoa wito wa kwa wafanyakazi wa vyombo vya maji kuwa waangalifu  wakati wanapo kuwa katika hali ya kulewa kutorudi katika vyombo vyao au kuacha kabisa kujihusisha na unywaji wa pombe kupita kiasi.

Nitoe wito kwa wafanya kazi wote wa vyombo vya majini kwamba wawe na tahadhari endapo wanapokuwa wapo katika hali ya kulewa kutorudi katika vyombo vyao walale hukohuko au wanunue pombe zao wakanywee katika vyombo vyao lakini pia niwaambie kwamba unywaji wa pombe kupita kiasi si salama sana kwahio wito wangu kwao kuwa na tahadhari sana katika hali hii kwamana inaweza kuleta madhara makubwa kama haya ambayo yamejitokeza ………alitoa wito huo mkuu wa upelelezi kutoka jeshi la polisi wilayani Pangani ASP-MATIKU

Chombo ambacho kumetokea Ajali hiyo kikiwa kimetia nanga karibu na Bandari ya Pangani, mita chache kutokea kilipo kituo cha Redio cha Pangani FM

Na mpaka sasa tayari mwili wa marehemu umeshachukuliwa na ndugu zake kwa shughuli za mazishi.