TAHADHARI ZAIDI YA CORONA BANDARI YA KIPUMBWI.

Uongozi wa serikali ya Kijiji cha Kipumbwi wilayani PanganiΒ  Mkoani Tanga umetakiwa kuweka mikakati ya kukabiliana na ugonjwa wa Corona ikiwemo uwepo wa maji ya kusafishia mikono eneo la Bandarini.

Hayo yamesemwa na  Kaimu mkuu wa Mkoa wa Tanga Bwana YONA MIKE katika ziara iliyohusisha viongozi wa kiserikali iliyohusisha vijiji vya Kipumbwi na Mkwaja.

β€œLakini mnatakiwa kunawa mikono wakati wowote,nyie hapa mnapata wageni wengi,kutokupeana mikono ni jambo la msingi kwa sasa haimaanishi kwamba mmepoteza upendo kwa kufanya hivyo,sasa mwenyekiti wa Kijiji ukiletewa na Mkurugenzi lile la kunawa hakikisha watu wana nawa Mkurugenzi hakikisha unalisimamia hilo”

Kwa upande wake Meneja Bandari ya Kipumbwi Bwana STEVEN ELIMBAKWENI amesema bado kuna changamotoΒ  ya watu kutumia njia za panyaΒ  hivyo elimu inahitajika zaidi kwaniΒ  mbali na mapambano dhidi ya CORONA huchangia upotevu wa mapato ya serikali.

β€œSisi Bandari bubu tuliziua na kuzirasimisha ikiwemo hii ya Kipumbwi,lakini bado kumetokea sehemu nyingine ambazo watu wamekuwa wakipita,elimu pia izidi kutolewa kwa wale ambao wanakwepa basi hatua zisiwe ndogo”

Ziara hiyo iliyohusisha viongozi wa serikali kutoka ndani na nje ya wilaya ya Pangani iilikuwa na lengo la kutoa elimu kwa wananchi wa vijiji vya Kipumbwi na Mkwaja juu ya ugonjwa wa CORONA ukizingatia uwepo wa Bandari katika vijiji hivyo kusababisha kuingia kwa watu.