Vijana Wilayani Pangani Mkoani Tanga wametakiwa kujitokeza katika kushiriki mafunzo ya uokozi ambayo yantolewa na jeshi la zima moto

Mafunzo hayo yanatolewa katika eneo la ofisi ya kijiji cha pangani Pangani Mashariki ambapo jeshi hilo limekutanisha vijana mbali mbali kutoka wilayani humu.

Akizungumza na pangani FM katika eneo la mafunzo hayo, coordinator wa mafunzo SAJENTI HALFANI MUHINA amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kusaidia jamii endapo kunahitilafu inatokea kwenye eneo Fulani na pia vijana kuwajenga kuwa na tabia njema pamoja na ukakamavu wa mwili

Lengo au dhumuni halisi la mafunzo haya ni kurudisha uzalendo kwa vijana na kuwajengea ukakamavu wa mwili na nidhamu kwamana endapo mafunzo haya yatakapokwisha vijana hawa watarudi katika maeneo yao na watakuwa volunteer wa jeshi la zima moto na uokozi katika jamii .

Aidha amesema vijana hao watasaidia kutoa elimu ya namna ya uokozi na kuzima moto katika maeneo mbayao wanatoka.

Atakapotoka hapa kijana atakuwa ameiva kwa namna nyingi sana kwa tutakuwa na njia nyingi sana ya kukabiliana na majanga lakini itakuwa wao ni sehemu ya kutoa elimu juu ya majanga hayo katika jamii zao huku wanakouishi kwao sasa utaonatulicho lenga sisi ni jamii kuwa na uwelewa na huo uwelewa uingie Zaidi ndani ya jamii na wilaya kwa ujumla na kuhakikisha kwamba majanga haya tunayatokomeza.

Kwa upande wa vijana ambao wamejitokeza kupata mafunzo hayo wamesema kuwa ni mazuri huku wakiwashawishi vijana wenzao ambao wanahitaji kujiunga na mafunzo hayo.

Aaaah mafunzo ni mazuri tangu tuanze mazoezi haya yanakwenda vizuri na tumeyapokea kwa mikono miwili, kikubwa ni kujitahidi siku zote mwanzo huwa mgumu lakini kila siku zinavyokwenda miili inazidi kuyazoea mazoezi na vile vile kwa kupitia fursa hiii ni waambie vijana wenzangu ambao wanahitaji kujiunga na mafunzo haya kwamba wajitokeze na nafasi zipo kwamana mafunzo haya yanafaida kubwa katika jamii na tukiwa sisi kama vijana.

SAJENTI HALIFANI MUHINA amemalizia kwa kutoa wito kwa vijana kwa kujitambua na kuwa na mwamko wa kuwania fursa ambazo zinajitokeza katika jamii.

Wito wangu kijana kam kijana ajitambue na atambue kwamba fursa kama fursa inatokea kwa namna nyingi tunapo kutana hapa tunajifunza falsafa ya namna nyingi hatuishii kwenye mafunzo ya zima moto tu hapana tunatoa mafunzo ya ukakamavu wa mwili,kuwajenga kuwa na nidhamu nzuri kwa kuwa unaporudi unakuwa ni kijana mpya hata katika uwajibikaji kwamana cv ni kila kitu katika maisha yetu kwa hiii pia ni moja ya kujiongezea cv.

Na mafunzo hayo yatafanyika kwa muda wa wiki tatu katika eneo la ofisi ya pangani mashariki

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeundwa na kufanya kazi chini ya sheria namba 14 ya mwaka 2007 “FIRE AND RESCUE FORCE ACT”. Majukumu makubwa ya Jeshi ni kuzima moto na kuokoa maisha na mali katika majanga yatokanayo na moto, mafuriko, tetemeko la ardhi, ajali za barabarani pamoja na majanga mengineyo.