SHIRIKIZA LA UZIKWASA LATOA VIFAA KINGA NA VIFAA TIBA KWA HOSPITALI YA WILAYA YA PANGANI.

Shirika la UZIKWASA lililopo wilayani Pangani Mkoani Tanga leo limetoa vifaa kinga na vifaa tiba kwa hospital ya wilaya ya Pangani vyenye thamani ya shilingi 41,868,950 kwa ajili ya kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa wa corona.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo mkurugenzi wa shirika hilo bwana NOVATUS URASSA amesema kuwa kutokana na shughuli zao kusimama kwa muda kutokana na janga la corona kwa kushirikiana na wafadhili wao IRISH AID ndipo walipoelekeza bajeti ya shughuli hizo  katika sekta ya afya wilayani humo.

 ‘Kazi zetu sisi UZIKWASA huwa tunakutana na watu tunahitaji madarasa tunahitaji kufundisha na kazalika na ukijaribu kuangalia tangia mwezi wa tatu shughuli zetu ziliathirika na janga la corona kwasasbabu tusingeweza kuwaita watu na kuwapatia mafunzo kwahiyo tulichofanya ni kuwasiliana na wafadhili wetu na kuwaeleza hali ilivyo na kuwaambia kuwa shughuli sasa zimesimama, munaonaje hii bajeti tuliyoipanga tusielekeze kwa ajili ya shughuli, tuielekeze hospitali iweze kusaidi katika mapambano ya corona na baada ya kuongea nao vizuri wakakubali na ndipo tuka wasiliana na mganga mkuu kwa ajili ya vifaa ambavyo tuna uwezo navyo na tunaweza kuvichangia”

Akifikisha salamu kwa niaba ya mkuu wa wilaya katibu tawala wilayani hapa MWALIMU KHASAN NYANGE amelipongeza shirika hilo kwa kutoa vifaa hivyo.

UZIKWASA katika hili walilolifanya mkurugenzi analijua shilingi milioni arobaini na moja  mianane sitini na nane elfu ma miatisa na hamsini sio fedha ndogo katika uwekezaji wa sekta ya afya walikuwa wananaweza kutafuta alternative yoyote  huko vijijini na naimani hao wafadhili wao wangewaelewa lakini wao wakaona wanunuje hivi vifaa ili viende vikasaidie kupambana na janga la corona lakini pia vikasaidie kuokoa maisha ya watu eeh hiki tunachokifanya hapa ni miongoni mwa sehemu itakayotusaidia kutoa elimu huko tutakapokwenda”

Kwa upande wake mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Pangani ndugu ISAYA MBENJE ameeleza namna ambavyo halmashauri yake ilivyowashirikisha wadau katika mapambano ya Covid-19.

“Wakati harakati za kupambana na virusi vya corona zilivyopamba moto kama halmashauri tukaamua kuwasiliana na wadau mbalimbali kujaribu kuona wanaweza kutusaidia nguvu kwa maana ya vifaa vya kuweza kusaidia mapambano dhidi ya covid-19 tuliwasiliana na wenzetu wa UZIKWASA na wakaonesha nia kuwa watatusaidia kwa jinsi ambavyo wataweza kufanya na baadae wakatupigia simu kuwa katika kutafuta kutoka kwa wafadhili wao na wao wamefanikiwa kupata vifaa tiba  mchanganyiko kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya covid-19 lakini pia katika kutoa huduma za afya kwa ujumla”.

Mganga mkuu wa Wilaya ya Pangani DKT RASHIDI MAJALA amelishukuru shirika hilo kwa kujitolea vifaa hivyo huku akisema kitendo hicho kinawafariji watumishi wa idara ya afya huku akiahidi kuvitunza kwa ajili ya kuwasaidia wakazi wa Pangani katika mapambano ya janga la Corona.

“Kwa namna ya kipekee tumewashukuru sana wenzetu wa shirika la UZIKWASA kwa msaada huu mkubwa wa vifaa hivi kinga na vifaa tiba kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa COVID-19 kwahakika tumefarijika sana kama watumishi wa afya kwa maana ya kupata vifaa hivi na mimi kama mganga mkuu naahidi kuvitunza vifaa hivi na kuvitumia ili viweze kuwasaidia wananchi wa PANGANI”

Katika kuendelea kuielimisha jamii  kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Covid 19 shirika hilo pia limetoa memory card 66 na viakisi mwanga kwa bodaboda Wilayani Pangani

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *