MAZOEZI YA KIJESHI KATIKA FUKWE ZA BAHARI WILAYANI PANGANI, WANACHI WATAKIWA KUTOFIKA.

Wananchi Wilayani Pangani Mkoani Tanga wametakiwa kutofika katika Baadhi ya maeneo ya Bahari wilayani humo ili kupisha mazoezi ya kijeshi yatakayofanyika siku ya Kesho katika  Maeneo ya Kimang’a kuelekea Kigombe.

Agizo hilo limetolewa na Katibu Tawala wilaya ya Pangani Mwl. Hassan Nyange ambapo amewataka wananchi kutofika katika maeneo hayo hapo kesho ijumaa,Juni 26  kwakuwa mazoezi hayo yatahusisha matumizi  ya silaha za kijeshi  kuelekea Baharini.

Kesho tarehe 26  mwezi wa sita mwaka huu 2020 siku ya Ijumaa jeshi letu la ulinzi la wananchi JWTZ kutoka jijini Tanga wanategemea kufanya mazoezi ya majaribio ya makombora makubwa katika maeneo ya vijiji vya Kigombe, Kimang’a, Ziwani  na Vumbi, lakini baadhi ya maeneo ya vijiji vya pangani yataathirika kwa namna moja ama nyingine,  hivyo wavuvi wa kijiji cha Kimang’a na maeneo ya karibu kwa upande wa bahari kuelekea Kigombe maeneo hayo wasimamishe shughuli zote za uvuvi kwa siku ya kesho ili kupisha zoezi hilo litakaloanza mapema asubuhi hadi jioni. Amesema DAS Pangani.

Aidha Mwl. Nyange amewataka wananchi kuwa watulivu kwakuwa mazoezi hayo hayatakuwa na madhara.

Niwaombe watu wawe watulivu mizinga hiyo inayipigwa kuelekea baharini hayatawaathiri kwa namna moja ama nyingine isipokuwa maeneo yale ambayo tumeyataja ndiyo yatakuwa kuna athari huku kwengine kama watasikia makelele au miungurumo basi wawe watulivu tu hakuna lolote baya ambalo litakuwa linaendelea hivyo ndugu zetu wa pangani wanaofanya shughuli zao za uvuvi katika eneo la kimang’a na kigombe wasitishe shughuli zao hapo kesho.

Amesema DAS Pangani.

Mazoezi  hayo ya kijeshi yatafanywa na chuo cha mafunzo ya jeshi  kilichopo mjini Tanga kesho Ijumaa kuanzia majira ya asubuhi hadi jioni.