DAS PANGANI : WATAALAMU WA AFYA WAENDELEE KUTUMIA HEKIMA NA BUSARA ILI WAZEE WASIKOSE MATIBABU.-

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Pangani,Katibu Tawala (DAS) Wilaya ya Pangani Mwalimu HASSANI NYANGE hii leo wakati akizungumzia changamoto mbalimbali zinazowakumba wazee ikiwemo upatikanaji wa matibabu amesema serikali ipo katika mchakato wa kumalizia sheria ya wazee,ambapo imeonekana sera ya wazee na sera ya afya inakinzana na kupelekea changamoto katika utolewaji wa huduma za aafya kwa wazee.

“Kuhusu mgongano wa sera ya wazee na sera ya afya utamalizika pale sheria itakapokuwa imekamilika,(ambapo sera ya wazee inataja mzee ni kuanzia miaka 60,huku sera ya matibabu ikisema matibabu ni kwa wal wasiojiweza tu) hivyo kwa sasa niwaombe tu wataalamu wa afya waendelee kutumia hekima na busara ili wazee wasikose matibabu kabisa”

Hayo yamejiri katika Mchakato wa kuundwa kwa Baraza la wazee uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ambapo Umehudhuriwa na wawakilishi wa wazee kutoka kata kumi na nne wilayani pangani,wawakilishi kutoka shirika la AFRIWAG,ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Pangani akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya.