DAS PANGANI; HATUNA CHANGAMOTO KUBWA YA WAHAMIAJI HARAMU PANGANI

Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Pangani imempokea kamishina mkuu wa Jeshi la Uhamiaji nchini CGI Dokta Anna Makakala kwa lengo ni kuangalia changamoto mbalimbali zinazoikumba idara hiyo wilayani Pangani.

Akizungumza na Pangani fm  Katibu tawala wilayani Pangani Mwalimu Hassani Nyange amesema ujio wake  ni kwa ajili ya kuangalia shughuli za uhamiaji namna ya kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili.

 “Amekuja kuangalia hali halisi ya shughuli zinavyokwenda  za masuala ya uhamiaji na changamoto zake na namna tunavyoweza kuzitatua kwa pamoja”

Kwa upande mwengine mwalimu Nyange amesema  ingawa kwa wilaya ya Pangani hakuna changamoto kubwa ya kesi ya wahamiaji haramu,ila bado wataendelea kuhakikisha idara hivyo inafanya kazi yake ipasavyo.

 “Hatuna changamoto kubwa ya wahamiaji haramu tumekubaliana tunafanya kazi kwa kujituma kuhakikisha idara ya uhamiaji wilayani Pangani inakaa vizzuri”

ziara hiyo ya kikazi ya Kamishina mkuu wa uhamiaji nchini ni shemu ya Ziara zake nchini ambapo aliambatana na kamishina wa uhamiaji Mkoani Tanga,na kukutana na kamati ya ulinzi na usalama wilayani Pangani.