WEZI WAVUNJA NA KUIBA KWENYE NYUMBA YA MWALIMU SAA 10 JIONI

Kamanda wa Polisi Wilaya ya Pangani Bi. GEORGINA RICHARD MATAGI amethibitisha tukio la wizi uliohusisha kuvunjwa kwa nyumba ya mwalimu wa shule ya Sekondari ya Funguni iliyopo kata ya Pangani Magharibi Wilayani Pangani Mkoani Tanga

Akielezea zaidi kuhusiana na tukio hilo Bi Georgina amesema Jeshi la polisi limewakamata watu watatu wanaosaidikiwa kuhusika na tukio hilo ambapo amesema watu hao walikamatwa majira ya saa kumi jioni eneo la Miono wilayani Pangani wakiwa wamebeba vitu mbalimbali wakitokea mjini TANGA.

-“mnamo tarehe 6 Julai majira ya saa kumi jioni tulipata taarifa ya kuvunjwa nyumba ya mwalimu wa shule ya sekondari Funguni mwenye umri wa miaka 32 ambapo huyu mwizi ni rafiki wa mwalimu huyu na alifika siku tatu nyuma kwa ajili ya kumtembelea kumbe alikuja kuchora ramani ya nyumba ikoje.

”-Aidha bi GEORGINA amesema kuwa watu hao wamekamatwa katika eneo la kituo cha mafuta walipokuwa wanajaza mafuta ili wapate kuondoka ndipo watu wa maeneo hayo wakawashtukia na kutoa taarifa zilizofanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao na kufikishwa kituo cha Polisi.

-“kwahiyo baada ya kuondoka huyu mwizi alikwenda tanga kukodi bajaji na kusomba vitu vyote na wakati huo mwalimu yuko shule na huyu rafiki yake anajua mazingira ya pale nyumbani, wakati washapakiza vitu wakafika kituo cha mafuta ili waweke mafuta na kuondoka lakini wakati wamefika pale kituoni watu wakawa na wasiwasi kwa kuona bajaj isiyo ya maeneo ya pangani na sura za watu pia ni ngeni wakaanza kuwahoji na kuwapiga kwahiyo taarifa zikatufikia tukafika eneo la tukio na kukuta wamepigwa vibaya sana”“kwa hiyo baada ya kuondoka huyu mwizi alikwenda Tanga kukodi bajaji na kusomba vitu vyote na wakati huo mwalimu yuko shule na huyu rafiki yake anajua mazingira ya pale nyumbani, wakati washapakiza vitu wakafika kituo cha mafuta ili waweke mafuta na kuondoka lakini wakati wamefika pale kituoni watu wakawa na wasiwasi kwa kuona bajaj si isiyo ya maeneo ya pangani na sura za watu pia ni ngeni wakaanza kuwahoji na kuwapiga kwahiyo taarifa zikatufikia tukafika eneo la tukio na kukuta wamepigwa vibaya sana”

-Kufutaia tukio hilo Bi Georgina ametoa wito kwa jamii kuwa endapo watawakamata watu au kuwahisi kuwa ni wezi basi watoe taarifa sehemu husika na si kujichukulia sheria mkononi ili kilinda usalama wao na jamii kwa ujumla.