USAILI WA JKT WAMALIZIKA PANGANI DC KUTANGAZA TENA NAFASI ZA WASICHANA.

Kamati ya ulinzi na usalama wilayani Pangani Mkoani Tanga ikiongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo  leo imekamilisha zoezi la usaili kwa vijana watakaojiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) mwaka huu.

Baada ya kuhitimishwa kwa usaili huo, Mkuu wa wilaya ya Pangani BI ZAINAB ABDALLAH ISSA amewapongeza vijana waliojikeza kuomba nafasi hiyo na kuingia katika usaili kwakuwa inaonesha ari na uzalendo kwa taifa lao.

Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi.Zainab Abdallah pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bw. Hasani Nyange katika zoezi la Usaili.

Akitangaza  matokeo ya usaili huo Bi ZAINABU amewataja vijana waliopita katika mchujo wa awali huku akitangaza nafasi zilizo wazi kwa wasichana kwa upande wa wahitimu wa darasa la saba , kidato cha sita na wahitimu wa vyuo.

“Darasa la saba nafasi za wavulana zilikuwa tatu na za wasichana zilikuwa tatu kwa bahati mbaya hakuna hata msichana mmoja aliyejitokeza kwahiyo tumekubaliana kuwa tutatangaza tena hizi nafasi za wasichana na form six nafasi zilikuwa mbili kwa wavulana na kwa wasichana ilikuwa ni moja lakini hakuna msichana aliyejitokeza, stashahada na shahada nafasi kwa wanawake zilikuwa ni mbili lakini aliyeomba ni mmoja na amepita kwenye mchujo kwa hiyo nafasi moja imebaki”.Amesema Bi ZAINABU .

Kwa upande wake Katibu tawala wilaya ya Pangani Bw. HASSAN NYANGE amesema kuwa mchakato wa kuwapata vijana hao ulikuwa ni wa haki na kuongeza kuwa watatangaza tena fursa yausaili kwa vijana ili kuziba nafasi zilizo wazi.

“Zoezi lilikuwa ni la haki na mfumo ulikuwa ni kuandika maksi kwa siri kwahiyo ilikuwa ni ngumu kumpendelea mtu na nimeandika tangazo kwa ajili ya kutangaza tena nafasi ili kuziba nafasi zilizo achwa wazi”.Amesema Mwl. HASSAN NYANGE.

Pia Mwl. HASSAN NYANGE ameelezea kusikitishwa kwake na tabia ya baadhi ya watu kufoji vyeti akisema ni jambo lisilofaa lisilovumilika.

“Kumekuwa na changamoto kubwa sana ya kufoji vyeti sisi hatuwezi kuvumilia suala la kufoji vyeti hivyo tunawaomba wanapangani waendelee kuwasisitiza vijana wao na kuna wazazi tuliwaita mbele ya kamati ya ulinzi na usalama tuombe watu watende haki na wahakikishe kuwa wana vigezo vinavyotakiwa ili ili tunapoenda mkoani vijana wetu wote wapite.” Ameongezea Mwalimu Nyange.

Zoezi la kuwapata vijana hao lilianza kwa kutolewa kwa matangazo katika kila kijiji kuanzia mwishoni mwa mwezi wa nane hivyo vijana hao waliopata nafasi wataingia katika awamu ya pili ya mchakato hapo kesho kabla ya kufika mkoani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *