WANANCHI MADANGA WALALAMIKIA UBOVU WA BARABARA YA MWEMBENI-BUSHIRI

Wananchi wa kijiji cha Madanga Wilayani Pangani Mkoani Tanga wamelalamikia ubovu wa barabara kutoka eneo la Mwembeni Madanga hadi Bushiri hali inayopelekea mabasi ya abiria kutofika kijijini hapo na kuleta usumbufu kwa wananchi hao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema hali hiyo imekuwa ikiwaathiri kiuchumi kwani  hulazimika kutoa nauli marambili ukilinganisha na kipato chao.

hali ya miundo mbinu ya barabara ya mwembeni-madanga-kimang’a ni mbaya sana ni adha kubwa kwetu na ni kero ,magari hayapiti kwasababu ya barabara abiria anatoka madanga anapanda bodaboda mpaka mwembeni au bushiri atoe shilingi elfumbili kwenda na kurudi elfu nne bado nauli’.wafanyabiashara wanapata shida kusafirisha biashara zao ,wakina mama pia wanapata adha kubwa’’,wamesema wananchi hao.

DEODATUS SHANEL ni kondata wa moja ya mabasi yanayofanya safari zake Pangani ,Muheza amekiri kutofika katika kijiji cha Madanga huku sababu kuu wakiitaja miundo mbinu ya barabara.

’Kweli tunawaudhi abiria wetu ila nao pia wameshaelewa kwamba kikwazo ni barabara na barabara zikiwa nzuri tutafika kwani  wanapata tabu sana ,barabara zikirekebishwa tutafika madanga”.amesema kondakta huyo

kufuatia hayo Pangani FM Radio imefika katika Ofisi za wakala ya barabara Vijijini na mijini (Tarura) Wilayani Pangani na kuzungumza na meneja wake Mhandisi ELIA MGAYA ambae ameeleza jitihada wanazozifanya katika matengenezo ya barabara hiyo licha ya kukosa bajeti huku akiwataka wananchi wa Madanga kuwa na subra katika suala hilo.

’Kiukweli barabara ya Mwembeni-Mdanga -Bushiri haikupata Fungu katika mwaka wa fedha 2019-2020 lakini sisi kama TARURA tumebuni vyanzo vya mapato na tukaifanyia matengenezo kidogo,na hii ni kutokana na kwamba katika mwaka huo wa fedha pesa nyingi tulizielekeza kwenye ujenzi wa barabara zetu tunazojenga na halmashauri kwa mapato ya ndani, kwa sasa wananchi wawe na subira washirikiane na tarura ili tupange mipango ya pamoja,na kwa mwaka wa fedha 2020-21 barabara zote ambazo zilikuwepo kwa mwaka 2019-2020 na zilifanyiwa matengenezo kidogo zitafanyiwa matengenezo licha ya kuwa barabara hiyo haina bajeti lakini tunaweza tukatafuta namna ya kufanya tukaifungua kidogokidogo’’Amesema Mhandisi ELIA

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) ni Wakala katika Wizara chini ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

Jukumu kubwa la Wakala ni usimamizi, ujenzi, na matengenezo ya mtandao wa barabara za vijijini na mijini ikijumuisha kuimarisha usalama wa barabara, kulinda hifadhi za barabara zisivamiwe na kudhibiti athari za mazingira na za kijamii.