TAKUKURU YAFANIKIWA KUOKOA NA KUREJESHA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 12 ZA SACCOS YA VIJANA PANGANI.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Pangani mkoani Tanga imefanikiwa kuokoa na kuwarejeshea fedha Wananchi kutoka kwenye uongozi wa zamani wa SACOSS ya UMOJA WA VIJANA PANGANI (UVIPASA).

Fedha hizo ni Shilingi Milioni Kumi na sita laki tano Themanini na Tano Elfu,Mia Nne Arobaini na Tatu (12,585,443/=) ambazo zilitolewa na Halmashauri  ya Wilaya ya Pangani mnamo mwaka 2013.

Hapo jana 10/9/2020 mkuu wa Takukuru wilayani Pangani DIAMON MWAKABABU akiambatana  na kaimu mkuu wa takukuru Mkoa wa Tanga DKT Sharifa Bungala wamefanikiwa kukabidhi sh. 12,185,443 kwa SACCOS ya umoja wa vijana UVIPASA Pangani

Fedha zilizokabidhiwa kwa UVIPASA Tsh 12,185,443 ni ambazo zilitolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Pangani mnamo mwaka 2013 kwa ajili ya kuwawezesha vijana kukopa ili kuinua mitaji ya Biashara zao lakini viongozi hao hawakurudisha fedha hizo kwa zaidi ya takribani miaka 6 (2014-2020) Baada ya TAKUKURU Pangani kuingilia kati na Uchunguzi kufanyika fedha hizo zilirudishwa.

operesheni hiyo imefanyika kutokana na malalamiko yaliyowasilishwa TAKUKURU Mkoa wa Tanga baada ya wanachama wa SACCOS wakiwalalamikia baadhi ya wanachama na viongozi wa Umoja huo kuchukua mikopo kwenye Chama hicho tangu mwaka 2014 na kukaidi kurejesha kwa zaidi ya miaka 6 hali iliyopelekea SACCOS hiyo kushindwa kujiendesha ikiwemo kutorejesha akiba za wanachama wanaojitoa au kupunguza hisa zao.

Pamoja na kukabidhi fedha hizo TAKUKURU Wilaya ya Pangani bado inaendelea kuwatafuta viongozi na Wanachama wa SACCOS hiyo ambao bado wanadaiwa na Pia imetia agizo kwa wale wanaodaiwa kujisalimisha na kurejesha fedha hizo katika Ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Pangani.