WANAFUNZI 1379 WILAYANI PANGANI WANATARAJIA KUFANYA MTIHANI WA DARASA LA MWAKA 2020.

Wazazi na walimu wilayani Pangani Mkoani Tanga wametakiwa kuwawezesha kimasomo wanafunzi wanaotarajiwa kufanya mitihani ya Darasa la saba mwezi Oktoba Mwaka huu ili kuongeza kiwango cha ufaulu.

Akizungumza na Pangani FM ofisini kwake mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Pangani ndugu ISAYA MBENJE amesema kuwa mitihani ya kuhitimu darasa saba mwaka huu wa 2020 inatarajiwa kufanyika tarehe saba na nane ya mwezi October

’Niwajuze wananchi wa pangani kwamba kuanzia tarehe saba na tarehe nane ya mwezi wa kumi tutafanya Mitihani ya kuhitimu Elimu ya Msingi na kama tunavyofahamu, vijana wetu wako busy wanafanya maandalizi, kwa hiyo naomba Wazazi na Walimu waendelee kuwawezesha Vijana wetu waendelee kufanya hiyo  Mitihani, watu wengi wanafikiri kufaulu Mitihani inatokea ghafla, haitokei hivyo bali ni maandalizi na Vijana wetu wameshaandaliwa vya kutosha na walimu wao na niwasihi tuuu walimu watakaoteuliwa kusimamia mitihani wafanye kazi yao kwa ufanisi’’ amesema ndugu Isaya Mbenje.

Aidha Bw. MBENJE amewataka wazazi kuweka utaratibu mzuri kwa wahitimu hao kupata chakula kitakachowasaidia kuwa makini na mitihani na kumalizia kuwa ni vyema kuanzia sasa wakaandaliwa kisaikolojia ili kuwawezesha kupata matokeo mazuri.

Mitihani ya kuhitimu darasa la saba hufanyika kwa siku mbili mfululuzo Nchini ambapo kwa wilaya ya pangani jumla ya watahiniwa 1379 wanatarajiwa kufanya mtihani huo huku wasichana wakiwa 698 na wavulana ni 981.