PANGANI FM YAENDELEA KUWA KIDEDEA TUZO ZA UMAHIRI WA UANDISHI WA HABARI NCHINI (EJAT)

Mwandishi wa Habari toka kituo cha Radio Pangani FM Rajabu Mustapha Mrope ametangazwa mshindi katika Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania EJAT kwa Mwaka 2019 katika kipengele cha Utalii.

Tuzo hizo ambazo hutolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT)

Mwaka huu Kazi zaidi ya 400 zilipokelewa na kushindanishwa.

Tukio la ugawaji wa Tuzo hizo limefanyika Usiku wa Septembea 28 katika Hoteli ya Tanga Beach Resort likihudhuriwa na waandishi wa Habari toka Mikoa mbalimbali Nchini, wadau wa Habari, viongozi wa Taasisi binafsi na Serikali huku Mgeni Rasmi akiwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh, Martin Shigela.