VIONGOZI 50 WA DINI MBALIMBALI PANGANI WAMELISHUKURU SHIRIKA LA UZIKWASA KWA MAFUNZO YA UONGOZI WA MGUSO.

Viongozi 50 wa dini mbalimbali wilayani Pangani Mkoani Tanga wamelishukuru shirika la UZIKWASA kwa mafunzo waliyopatiwa na shirika hilo na kusema kuwa yamewajengea uwezo wa kukabiliana na vitendo vya ukatili vilivyopo katika maeneo yao.

Wakizungumza na kituo hiki mara baada ya kupatiwa mafunzo hayo viongozi hao wamesema kuwa uongozi ni dhamana waliyopewa na Mungu hivyo ni vyema kutumia vyeo vyao bila kubaguana ili kutatua vitendo vya ukatili.

“Mimi nilichojifunza ni kutengeneza maswali ya kujenga na sio maswali ya kulaumu kumbe kama viongozi wakati tatizo linapotokea tikitengeneza maswali ya kujenga tutatatua tatizo na tukibaki kulaumu kila siku tutarudi hapahapa hatutasonga mbele,pia nimefaidika kuwa tumekusanywa pamoja kuwa sisi ni wamoja hivyo tutumie elimu hii kwa wale ambao hawaende misikitini na makanisani ili kupata hofu ya mungu, lakini pia awali nilikuwa naona wapo watu wakufatilia ukatili mfano serikali,polisi na wengine mimi sihusika lakini kupitia semina hii kumbe nimetambua kuwa na mimi natakiwa nishiriki katika kufuatilia kesi za ukatili na kuzifuatilia”

Aidha kwa upande wake mchungaji GADIEL NAFTARI kutoka kanisa la EFATHA mjini pangani kwa niaba ya viongozi hao amelishukuru shirika la UZIKWSA kwa siku mbili kuweza kutoa elimu ya mguso ambayo itawasaidia kama viongozi kuisambaza katika jamii.

“nilishukuru shirika hili kwa elimu hii na ningependa kuliomba shirika la uzikwasa liendeleze moyo huu na bidii hii tukishirikiana kwa pamoja pangani itakuwa ile mungu ambayo anatamani kuiona iwe, ninaona kile kilichopo ndani ya moyo wa shirika hili kuwa wanavunja ukuta ambao upo katika nyoyo zetu hivyo tuyishi kama sisi ni wa moja na damu yetu moja”

Naye bi MAIMUNA MSANGI ambaye ni meneja wa kituo hiki, kwa niaba ya mkurugenzi wa shirika la UZIKWASA bwana NOVATUS URASA amewashukuru viongozi wa dini kwa kuitikia wito huo na kuwataka kuifanyia kazi elimu waliyopatiwa kwa siku mbili.

“tunawashukuru viongozi wa dini katika Imani zote kwa namna ambavyo mmeweza kuitikia wito wa kuweza kuwa nasi hapa na kuweza kushirikishana uzoefu wetu katika namna ambavyo tunashuhulikia masuala ya ukatili katika jamii zetu ili mwisho wa siku jamii yetu ikazidi kuwa salama kutokana na utatuzi usuhulishi au namna njema ambayo tutakwenda kuikuza kwa kupitia Imani ambayo tukonayo, tumekuwa tukidili na ukatili na kuhakikisha kwa tunaongezeana nguvu ili masuala haya na changamoto hizi ziende kwisha na ili mwisho wa siku jamii zetu zingie kwenye masuala ya stahiki”

Mafunzo ya uongozi wa mguso ni mafunzo ambayo yanamjenga kiongozi katika kujitafakari na kujimulika katika uongozi wake ndani ya familia nahata jamii kwa ujumla ili kupiga hatua za kimaendeleo na kuondokana na ukatili.