KARIBU MILIONI 500 ZATUMIKA KUKARABATI KIVUKO CHA MV PANGANI II

Katibu mkuu wa kitengo cha Ujenzi kutoka wizara ya  ujenzi  uchukuzi na mawasiliano nchini Tanzania Arch  ELIUS MWAKALINGA leo amezindua na kukabidhi kivuko cha Mv PANGANI II kwa wakala wa ufundi na umeme TEMESA Mkoa wa Tanga baada ya kufanyiwa ukarabati.

Akizungungumza wakati wa kuzindua na kukabidhi kivuko hicho lililofanyika katika eneo la feri Pangani mjini,  Arch  Mwakalinga ameiangaza TEMESA kuhakikisha wanasimamia vyema kivuko hicho huku akiwataka wananchi kushirikiana na serikali katika utunzaji wake ili kutimiza lengo lililokusudiwa.

‘Kwakuwa vivuko ni rasilimali muhimu ya taifa na vinahitaji na wananchi waliowengi hususani wa pangani ninawaagiza wakala wa TEMESA kuimarisha usimamizi na nyinyi wanachi kushirikiana na serikali ili hivi vivuko vitimize lengo lililokusudiwa.’ – Arch Mwakalinga

Aidha Mhandisi Mwakalinga amesema serikali imefanya ukarabati wa  Kivuko hicho ili kurahisisha usafiri kati ya mji wa pangani na miji iliyopo ng’ambo ya pili ya wilaya ya Pangani.

‘Vivuko hivi  vinarahisisha usafiri kwa watu wa pangani na vijiji vilivyopo ya ng’ambo ya mji wa pangani sasa kupitia vivuko hivi tunaweza kuwa na uhakika wa usafiri wa uhakika na usalama kwa watu wa pangani na kukuza biashara za watu wa pangani.’ – Arch Mwakalinga

Kwa upande wao wananchi wa pangani waliopata nafasi ya kuvuka na kivuko hicho wakati wa majaribio, wameishukuru serikali kwa kukikarabati kwakuwa itawapunguzia muda mwingi wa kusubiri kivuko kimoja.

‘Kwakweli tunaishukuru serikali kwa kukarabati kivuko hiki kitatusaidia katika kuvuka kwa wakati.” Amesma moja ya wananchi.

Kivuko cha mv pangani II  chenye urefu wa mita 30.76 na upana wa mita 7.10 kina uwezo wa kubeba magari madogo manne na watu mia moja ambapo ukarabati wake umegharimu kiasi cha shilingi milioni 496.01.