UZIKWASA YAWAKUTANISHA WADAU TOKA MASHIRIKA 16 MKOANI TANGA

Katika kuhakikisha vitendo vya ukatili vinapungua Mkoani tanga shirika la uzikwasa lililopo wilayani PANGANI, limewakutanisha wadau kutoka mashirika 16 Mkoani humo kwa lengo la kupata uelewa wa pamoja ili kutatua changamoto ya Ukatili.

Kufuatia mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoyakutanisha mashirika takribani 16 toka mkoani TANGA wadau hao wameweza kueleza changamoto wanazokutana nazo katika kufuatilia matukio ya ukatili kupitia mashirika yao.

“Pale tunaposhindwa kupata habari kwa undani kutokana na umri na jinsia kwa kuwa wakati mwingine anakuja Baba akinikuta mimi msichana hawezi kunieleza anaona aibu au utakuta pia anaweza kuja Mwanamke akimkuta Mwanaume pia hawezi kuzungumza anaona kuwa yeye Mwanamke amuelezee Mwanaume habari zake anaona haifai”

Wadau hao pia wameweza kuyaelezea mafunzo hayo na  namna yalivyoimarisha utendaji wao wa kazi kwa mtu mmoja mmoja  hata kwa mashirika yao.

“Mimi ni mara yangu ya kwanza kushiriki mafunzo ya ‘mguso’ mara ya kwanza walishiriki viongozi wangu lakini waliporudi waliweza kuyaambukiza kwa wafanyakazi wengine kwahiyo mimi nashukuru kwa mafunzo haya kwa kuwa naguswa na vitendo hivi kwakuwa ni Mwalimu pia kwahiyo wanafunzi wanakutana na ukatili hivyo nakaa nao na kuwapa elimu juu ya ukatili”

Aidha kwa upande wa bwana  ELIAS MSUYA ambaye ameteuliwa kuwa katibu wa kikao kazi kupitia mafunzo hayo  amesema kama wadau wa mapambano dhidi ya  ukatili ni vvyema kuwa na mawasiliano mazuri ili kushirikiana kwa pamoja.

Nafahamu kwa yale ambayo hatujayafanya ni muda sasa wa kutengeneza mawasiliano rafiki ili kukumbushana juu ya vitendo vya ukatili lazima tuwe na mtu kila wilaya ambaye atakuwa rahisi kutupatiua mrejesho wa matukio haya ili twende pamoja kulingana na ripoti ya ongezeko la matukio haya

Naye bwana DAUDI MLAHAGWA kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani amewashukuru wadau hao kwa kuitikia wito ambao utakwenda kuzaa matunda kwa mkoa wa Tanga.

“niwapongeze washiriki wa mafunzo haya kwa kuweza kuitikia wito wa warsha hii ambayo inatukumbusha tulipokosea na kutufanya tujione tulipo ili kuendeleza jitihada za kupambana na matukio haya lakini pia niwashukuru Shirika la UZIKWASA kwa kuendeleza kutoa Elimu hii na kuona wajibu wa Viongozi katika nafasi zetu hivyo kupitia mafunzao haya twende tukafanyie kazi changamoto ambazo tumeziweka kwenye mipango kazi yetu”

Kikosi kazi cha kupinga masuala ya ukatili kwa wanawake na watoto kimekutana kwa siku mbili katika ukumbi wa sea side uliopo hapa pangani mjini na kuandaa mpangokazi wa pamoja utakaowasaidia kuzifanyia kazi changamoto walizoziibua na kuzipatia ufumbuzi.