WAKULIMA WA MINAZI PANGANI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA.

Wakulima wa zao la Minazi Wilayani Pangani Mkoani Tanga wametakiwa kutumia Mvua za vuli kupanda Miche mipya ili kulifufua zao hilo wilayani humo.

Akizungumza wakati akiwa katika kipindi cha Makutano kinachorushwa na kituo hiki afisa kilimo Wilayani humu BW RAMADHANI ZUBERI amewataka wakulima kuchangamkia fursa ya miche ya minazi iliyopatikana kupitia kitua cha utafiti cha TARI kilichopo Mikocheni jijini Dar es salam kwa kushirikiana na wakulima wa zao la Minazi pangani

Pia bwana ZUBERI ameelezea kuwa kwa yeyote anaetaka kupata miche hiyo awasiliane na Afisa ugani wa kata yake ili kupata maelekezo huku akiongeza kuwa miche hiyo itapatikana kwa kuchangia shilingi elfu 2,000