
KAMATI ZA B.M.U WILAYANI PANGANI ZAING’ARISHA PANGANI KITAIFA.
Katibu mkuu wizara ya mifugo na uvuvi nchini Tanzania leo Novemba 16 2020 amefanya ziara ya siku moja wilayani pangani mkoani tanga na kukagua miradi na shughuli mbali mbali za uvuvi zinazoendelea wilayani humo .
Akiwa ziarani wilayani pangani katibu mkuu wizara ya mifugo na uvuvi Dk Rashidi Tamatamah amekagua ujenzi wa ofisi ya BMU katika kijiji cha kipumbwi unaotekelezwa kupitia mradi wa swiofish pamoja na soko la samaki lilipo katika kijiji cha pangani mashariki

Akizungumza na wananchi pamoja na viongozi wa BMU Dk. Tamatamah amesema kuwa dhumuni kubwa la kujenga ofisi za BMU ni kutokana na mchango mkubwa wa kamati hizo katika kusimamia rasilimali za uvuvi sanjari na kukusanya mapato
“BMU tumekuwa tukifanya nazo kazi kwa karibu sana na tangu tulipoanza kuwashirikisha katika ulinzi wa rasilimali za uvuvi matokeo yamekuwa makubwa sana kama mnavyo jua wizarani tuna kitengo kidogo sana na rasilimali hazitoshi kufika kila mahali hivyo hizi BMU zimetusaidia sana kulinda hizi rasilimali na hapa tumeonyeshwa nyavu ambazo wamezikamata nasisi tunapo pata muda huwa tunaungana nao kufanya hizi doria ”
Amesema Dk Tamahtamah
Dk Tamatamah amesema katika kukabiliana na changamoto ya matumizi zana duni za uvuvi ambazo zinawakosesha kipato wavuvi amesema ni vyema wavuvi hao kujiunga katika vyama vya ushirika ili iwerahisi kukopesheka
“mlionngelea wavuvi kuwa ni wanahitaji vyombo serikali tunafanya kazi na vikundi vya ushirika ambavyo vimesajiliwa kwanini tunahimiza hilo sisi rasilimali za wizara zinazotengwa ni ndogo kufanya kila kitu lakini tunafanya kazi na taasisi za kifedha kuna mabenki amabayo yanaweza kuwakopesha wavuvi ila jambo la msingi mnalopaswa kufanya ni kujiunga katika vyama vya ushirika ili iwe rahisi kukopesheka “
Amesema Dk Tamahtamah
Katika hatua nyingine katibu mkuu wizara ya mifugo na uvuvi ameipongeza halmashuri ya wilaya Pangani kwa kuzitumia vizuri kamati za bmu katika ukusanyaji wa mapato yatokanayo ya uvuvi
“nimefurahishwa kusikia baaada ya halmashuri kuwapa kazi ya kukusanya mapato mapato yameongezeka sana ..haya ni mafanikio makubwa na hivi ndivyo tunasisitiza kwa halmashuri nyingine nchini amabazo zinashughuli za uvuvi ziwape hizi kazi BMU ..na kwa mara nyingine ni shukuru wilaya ya pangani na ndio inayoongoza Tanzania kwa kuzipa hizi kazi bmu na matokeo yanaonekana “
Amesema Dk Tamahtamah