MIAKA 10 GEREZANI KWA KUJARIBU KUBAKA.

Mahakama ya Wilaya Pangani imemuhukumu mtu mmoja mwanaume anayefahamika kwa jina TUMAINI WILLIAM maarufu kama ALAS LOLIOSE,kifungo cha miaka 10 gerezani baada ya kupatikana na hatia katika mashtaka kujaribu kubaka pamoja na shambulio la aibu.

Hukumu hiyo imetolewa Oktoba 10 2020.

katika hati ya mshataka iliyowasilishwa mahakamani hapo inadaiwa kuwa kuwa mnamo tarehe 7/4 mwaka 2020 mshtakiwa huyo alifanya jaribio la kumbaka mwanamke mwenye umri wa miaka 25.

Hivyo Mshtakiwa amekutwa na makosa mawili moja ni jaribio la kubaka na la pili ni kufanya shambulio la aibu kwani alimvua nguo msichana huyo.