UCHAFU KATIKA MASHAMBA YA KOROSHO PWANI WATAJWA KUATHIRI UBORA WA ZAO HILO.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo kwa wakulima na maafisa uagani wilayani humo bi JANE .L. NINDI ambaye ni Afisa mdhibiti ubora wa bodi ya korosho mbali na ushauri huo pia ameitaja changamoto ya wakulima kutokuwa na ufuatiliaji mzuri wa mashamba yao jambo ambalo linawakwamisha katika uzalishaji wa zao hilo.

Tumeona kuna changamoto kubwa kwa mkoa wa Pwani na Tanga kwa wilaya zote hata hapa Pangani mashamba mengi ni machafu na korosho inapoanguka katika maeneo machafu hii ni maana kwamba tunakwenda kuzalisha  korosho ambayo siyo bora kwa hiyo tunasisitiza wakulima wote  wasafishe mashamba ili mwisho wa siku tupate korosho bora bei nzuri na wakulima wafurahie kilimo cha korosho katika Wilaya ya Pangani na Mkoa wa Tanga.

Amesema Bi.Jane

Naye bwana SAMSON ZABRON NGAMBA ambaye ni mtafiti wa uundaji wa shamba kutoka kituo cha TARI-NALIENDELE kwa upande wake amewataka wakulima hao wajikite katika kilimo mseto ambacho kitawawezesha kumuinua mkulima na kukuza uchumi wa taifa.

Tunawashauri wanapoanza kuaanda mashamba yao wazingatie vitu vyote ambavyo sio zao la korosho na lengo ni kufanya kilimo kiwe ni kilimo mseto na kilimo ili tuvutie soko la korosho katika mkoa wetu wa Tanga na korosho itajenga uchumi wa Tanga na uchumi wa wakulima na taifa kwa ujumla.

Akiwawakilisha wakulima na wataalamu wa kilimo waliohudhuria mafunzo bwana RAJABU KIROKA ambaye ni afisa ugani kata ya Masaika amewaomba watafiti kuendelea kuwatembelea mara kwa mara ili kuona kile walichowaelimisha na namna wanavyokifanyia kazi.

Tunawaahidi kuwa elimu hii tutaifanyia kazi lakini muwe mnatukumbuke kwa namna moja amna nyingine.

Amesema bwana Kiroba

Mafunzo hayo ya siku mbili ambayo yameanza siku ya jumatatu Novemba 16 kwa muundo wa nadharia na kufikia tamati siku ya jumanne Novemba 17 kwa vitendo ambapo wakulima wamepata nafasi ya kukutana shambani na kuona hatua mbali mbali za uundaji wa zao la korosho.