WAWILI WAFUNGWA MAISHA KWA MAKOSA YA UBAKAJI PANGANI.

Mahakama ya wilaya ya Pangani Mkoani Tanga imemhukumu mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina MBWANA SEFU mwenye umri wa miaka 28 kifungo cha maisha gerezani baada ya kupatikana na hatia katika shtaka la ubakaji.

Hukumu hiyo imetolewa Novemba 5 2020.

Katika hati ya mashataka iliyowasilshwa na hakimu mahakamani hapo ilidaiwa kuwa mnamo  tarehe 8-9 mwaka 2019 ndani ya wilaya ya Pangani mshatakiwa huyo alimbaka mtoto wa miaka 5 huku akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Katika hatua nyingine mahakama hiyo pia imemuhukumu mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina JOSEPH MASHAURI mwenye umri wa miaka 45 kifungo cha maisha gerezani baada ya kupatikana na hatia katika shtaka la ubakaji.

Katika hati ya mashtaka iliyowasilishwa Mahakamani hapo ilidaiwa kuwa mnamo Mwezi June hadi September mwaka 2019,katika eneo la Kimang’a Wilayani humo mshtakiwa alimbaka mtoto wa miaka 9 ambaye ni mwanafunzi wa shule ya Msingi wilayani Pangani.

Hukumu hiyo imetolewa Oktoba 10 2020 .