BWENI YAIBUKA MSHINDI KIJIJI BORA PANGANI 2020.

Kijiji  cha cha Bweni wilayani Pangani mkoani Tanga kimeibuka kuwa washindi kwenye shindano la Kijiji bora linaloratibiwa na shirika la UZIKWASA.

Tamasha la ugawaji tuzo kwa ajili ya Vijiji bora katika mapambano dhidi ya ukatili wa wanawake  na watoto wilayani Pangani limefanyika Leo Novemba 20 katika viwanja vya Bomani,ambapo  mgeni rasmi alikuwa Katibu tawala wa Wilaya ya Pangani Mwalimu HASSANI NYANGE kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi. ZAINAB ABDALLAH.

Katika Hotuba yake Mwalimu Nyange amesema watoto ndio kizazi kijacho hivyo mapambano dhidi ya Ukatili  ni jambo la msingi na la kuzingatiwa na kila mtu ili kutengeneza kizazi na Taifa bora.

Katibu tawala wa Wilaya ya Pangani Mwalimu HASSANI NYANGE

Aidha Mwalimu Nyange amesema ustawi wa watoto kwa musatakabali wa Kizazi Kijacho unategemeana na namna  jamii ya sasa itakavyowaandaa

,”kama taifa lina vijana wengi wanabakwa vijana wengi wamelawitiwa ,sasa lazima wataathirika kisaikolojia hivyo tutengeneze kizazi imara kwa ajili ya Taifa la kesho”

Pia  Mwalimu HASSANI NYANGE amesema jamii isischukulie matukio ya ukatili kama jambo la mtu binafsi na kuviomba vyombo vingine kama jeshi la polisi na Mahakama  kuendelea kusimamia haki ili  iweze kutendeka.

Kwa upande wao baadhi ya wanakamati wa MTAKUWA ya Kijiji cha Bweni wameelezea namna mafanikio yao yaliyopelekea kuibuka washindi

“Mwaka uliopita tulikuwa nafasi ya 4 tunashukuru mwaka huu tumekuwa washindi,lakini hatutabweteka tunaamini 2021 turudi tena kwenye nafasi yetu,aliongea mmoja ya mwanakamati wa MTAKUWWA Kijiji cha Bweni wakati wa utoaji wa tuzo kwa Kijiji Bora kwa mwaka huuu 2020.

Kwa kushika nafasi hiyo ya kwanza Kijiji cha Bweni kimepata zawadi ya shilingi laki 8,tuzo na cheti kutoka shirika la UZIKWASA ambao ni waratibu wa mashindano hayo.

Orodha ya Washindi ni Kama ifuatavyo;

 1. Bweni (Zawadi Tuzo na Fedha Tsh 800,000)
 2. Kimang’a(Zawadi Tsh 700,000)
 3. Stahabu (Zawadi Tsh 600,000)
 4. Mbulizaga (Zawadi Tsh 500,00)
 5. Mseko (Zawadi Ths 450,000)
 6. Mkwaja (Zawadi Tsh 450,000)
 7. Mtonga (Zawadi 300,000)
 8. Ushongo (Zawadi 300,000)
 9. Msaraza (Zawadi Tsh 250,000)
 10. Sange (Zawadi Tsh 200,000)

UZIKWASA ni shirika lenye uzoefu wa muda mrefu katika masuala ya usawa wa kijinsia, na programu za mabadiliko ya kijamii Tanzania. 

Mahindano hayo ambayo yameanzishwa mwaka 2010 hukutanisha wadau mbalimbali ndani na nje ya Pangani wakiwemo mamia ya Wananchi toka vijiji vyote vya Pangani wanaojitokeza kushududia Tamasha la utoaji wa Tuzo.

vigezo vilivyotumika kuwapata washindi ni kama ifuatavyo;

Vigezo vinavyotumika  kupata kijiji bora ni kama ifuatavyo;

 1. Mipango kazi jumuishi ambayo imebeba mafaniko yaliyopita na yale yanayotarijiwa kufanyika
 2. Ushirikiano wa makundi mbali mbali kama vile kamati ya shule, MTAKUWWA, VMAC, uongozi wa kijiji, polisi kata/polisi jamii, vikundi vya vijana& wanawake, wawezeshaji ngazi ya jamii na wadau mbali mbali kwa pamoja  katika kugawana majukumu ya utekelezaji wa mipango kazi
 3. Idadi ya afua/ shughuli zilizopo na zilizotekelezwa
 4. Mkakati wa kuishirikisha jamii katika utekelezaji wa mpango kazi
 5. kuwepo kwa kumbukumbu za taarifa za matukio ya ukatili katika ngazi ya kijiji, mashuleni na kwa wawezeshaji jamii.
 6. Vikao vya robo mwaka na muhtasari wake
 7. Idadi ya kesi ambapo jamii pamoja na kamati mbali mbali wamewezesha kwa namna zifuatazo
 8. Kutoa taarifa sahihi za kesi katika vyombo husika vya sharia
 9.  Kutoa taarifa sahihi za kesi/ tukio
 10. Kutoa ushahidi polisi/ mahakamani
 11. Kufuatilia hali ya kesi
 1. Idadi ya wanawake katika ngazi za uongozi
 2. Mikakati iliyopo na ambayo imeshatekelezwa ya kusaida makundi maalum ndani ya jamii mf: walemavu, wazee, yatima, wajane n.k