TAKUKURU PANGANI BEGA KWA BEGA NA USHIRIKA KUIFUFUA ‘UVIPASA’

Wanachama wa  SACCOS ya vijana wilayani pangani mkoani tanga (UVIPASA) wametakiwa kujitokeza kuwania nafasi mbali mbali za uongozi ilikuhakisha SACOSS hiyo inakua endelevu na kuwanufaisha wananchi kiuchumi.

Wito huo umetolewa na afisa ushirika wilayani pangani bwana Johson kaaya ambapo amesema kuwa uchaguzi huo unalenga kuwapata viongozi imara watakao simamia ushirika huo ambao uliyumba  kutokana na wananchama wasio waaminifu kushindwa kurejesha mikopo yao.

Aidha bwana Kaaya ameongeza kuwa vyama vya ushirika vinalenga kuwakwamua wananchi na kuwasisitiza wananchama wa sacoss ya vijana uvipasa kujitokeza katika mkutano  wa dharura utakaofanyika viwanja vya bomani tarehe 1/12/2020

Kwa upande wake  mratibu wa elimu kwa umma kutoka taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU wilayani pangani mbali na kueleza namna taasisi hiyo ilivyofanikisha kuokoa fedha za ushirika huo amewataka wananchi kuachana na vitendo vya rushwa

Mapema mwezi september Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Pangani ilifanikiwa kuokoa na kuwarejeshea  Wananchi kiasi cha Fedha zaidi ya Shilingi Milioni 12 kutoka kwenye uongozi wa zamani wa SACOSS ya UMOJA WA VIJANA PANGANI (UVIPASA) ambazo zilikopwa na baadhi ya wananchama na viongozi kisha kukaidi kurejesha .

Soma habari ya Takukuru kurudisha pesa za UVIPASA hapa chini. .