JESHI LA POLISI PANGANI LAVALIA NJUGA SWALA LA UKATILI KWA WATOTO.

Jeshi la Polisi Wilayani Pangani Mkoani Tanga limeanza zoezi maalum la kutoa elimu ya mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto wilayani humo.

Zoezi hilo limejiri kama hatua dhidi ya kuongezeka kwa matukio ya ukatili Wilayani humo.Siku za karibuni Jeshi hilo limewashikilia watu kadhaa kwa tuhuma za ubakaji kwa watoto na Mahakama Wilayani humo imetoa hukumu kadhaa zinazotokana na makosa ya ubakaji,shambulio la aibu na jaribio la kubaka.

Akizungumza katika zoezi hilo ambalo kwa siku ya kwanza limefanyika katika Eneo la Shule ya Msingi Boza Mkuu wa upelelezi kutoka jeshi la polisi wilayani pangani Ndugu, ELIJA MATIKU, amepongeza kwa mwitikio mzuri wa wanajamii katika kikao hicho na kusema kuwa kwa sasa jamii inakwenda kuwa na nguvu kubwa katika kuhakisha vitendo hivyo vinatokomea ndani ya jamii ya boza.

Naye mwezeshaji kutoka shirika la Uzikwasa Bwana NICKSON LUTENDA, amesema kuwa makuzi ya mtoto yanahihaji ushirikiano mkubwa miongoni mwa wanajamii.