HOSPITALI YA PANGANI YAPATA MASHINE YA X-RAY

Baada ya kusubiri kwa muda mrefu hatimaye Hospitali ya Halmashauri ya wilaya ya Pangani itaanza kutoa huduma ya  X-Ray baada ya kukabidhiwa rasmi ashine ya huduma hiyo.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mganga Mkuu Wilaya ya Pangani Bwana Maulid Majala amesema kwa sasa wananchi watapata huduma  bora na nzuri hivyo itapunguza rufaa za kwenda hospitali ya mkoa.

kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani  Bwana Isaya Mbenje amewataka wananchi  kujenga imani na Hospitali hiyo ya halmashauri ya wilaya ya Pangani kwani kwa sasa inajitosheleza kihuduma ambapo mbali na hayo pia amewashukuru wadau wengine waliosaidia upatikanajai wa X-RAY hiyo.

“Kama ambavyo mumewahi kusikia halamshauri nyingine zimepatiwa  X-RAY na sasa ni zamu ya Pangani,hivyo shukrani za dhati ziende kwa wizara ya afya,TAMISEMI,na wadau wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine” ameongeza Bwana Mbenje.

Kwa muda mrefu Hospitali ya Halmshauri ya wilaya ya Pangani ilikuwa inakosa huduma ya X-Ray na hiyo ilikuwa inawafanya wagonjwa waliokuwa wnahitaji huduma hiyo kuifuata katka hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo jambo ambalo lilikuwa linawaongezea wananchi gharama.