Tanga-UWASA YATOLEA UFAFANUZI KUKATIKA KWA MAJI PANGANI

Wananchi wilayani Pangani Mkoani Tanga wametakiwa kuwa wavumilivu kutokana na changamoto ya kukatika kwa umeme ambayo imepelekea changamoto ya upatikanaji wa maji kutokuwa katika baadhi ya maeneo wilayni humo

Akitoa taarifa kwa wananchi meneja wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Pangani bwana FUSI JOHN amesema kuwa kuanzia tarehe 19 mwezi huu hali ya upatikanaji wa Maji imekuwa si ya kuridhisha kutokana na hitililafu ya Umeme.

Kutokana na changamoto hiyo kwa niaba ya Mamlaka Meneja huyo ameomba radhi wananchi na kusema kuwa kama Tanga UWASA inasikitika kwa usumbufu uliojitokeza.

Hata hivyo Meneja huyo amesema kuwa watajaza maji kwenye visima vya kuhifadhia pale umeme utakaporejea leo hivyo amewataka Watumiaji wa huduma hiyo kuyakinga kuanzia Asubuhi ya kesho.

Maeneo yakatayoathiriwa na upatikanaji wa maji ni eneo la PANGANI mjinI ,BOZA na kwa wote wanaotumia kisima cha kusukumia maji cha BOZA