IDADI KUBWA YA WACHEZAJI WA KIGENI YATAJWA KUDIDIMIZA SOKA LA PANGANI.

Katika kusaidia kukuza soka la wilaya,Kocha mkuu wa timu ya ‘SAKURA KIDS Bwana Joackim Raphael amesema miongoni mwa vitu vinavyouwa mpira wa Pangani kwa sasa ni pamoja na baadhi ya timu kutumia idadi kubwa ya wachezaji wa kigeni kwenye Ligi zinazoendelea wilayani Pangani hivyo kunyima nafasi kwa vijana wazawa kuonyesha vipaji na uwezo wao.

Kocha huyo ameyazungumza hayo mara baada ya kuiongoza timu yake kuchukua ubingwa katika mashindano ya kuukaribisha mwaka 2021 katika mchezo wa fainali ulioikutanisha timu yake ya SAKURA KIDS ya Kwakibuyu na WADACHI FC ya Kipumbwi.

Kwa upande mwengine  ameomba ushirkiano kamili kutoka chama cha mpira wa miguu wilayani Pangani PDFA katika kuhakikisha wanakuwa bega kwa began na vilabu mbalimbali wilayani Pangani ili kuhakikisha vinapiga hatua,

”Tunawaomba PDFA wawe wanatafuta namna ya kukaa na sisi kama vilabu pamoja kuweza kujadili masuala ya Soka Pangani,kwa sababu sasa hivi mpira wetu umeshuka sana wilayani Pangani tofauti na kipindi chetu tulipkuwa tunacheza mpira”

Amesema Bwana Joackim Raphael